A song made by Owiti Arwa Chitu
A song made by Owiti Arwa Chitu
Chituz
*Yesu wa Miujiza*
Ninapotaka kukata kiu yangu,
Nitakimbilia kwako kwanza
Yesu wangu,
Hata nikiwa na ndugu zangu,
Geuza hali hii kuwa kama ile ya Harusi ya Kana.
Ulipogeuza maji watu wakafurahi Sana.
Wewe ni Yesu wa miujiza.
Wewe ni suluhisho kwa matatizo yote duniani,
Na neno lako asilani,
Linaweza kugeuza hali Fulani
kutoka mbaya na kuifanya ya furaha.
Ninapokuwa na familia yangu,
Na hatuwezi kupata chakula kwangu,
Mambo ni mabaya sana tangu,
Hatuwezi kumudu chochote tu mabangubangu,
Geuza hali hii kuwa kama ile ya kulisha watu 5000
Mikate mitano na samaki wawili
Wewe ni Yesu wa miujiza.
Wewe ni suluhisho kwa matatizo yote duniani,
Na neno lako asilani
Linaweza kugeuza hali fulani
Kutoka mbaya na kuifanya ya furaha.
Kunaponyesha mvua na kusababisha mafuriko,
Mvua nyingi radi na mitetemeko,
Nyumba zimesombwa vyombo,vijiko
Miko na majiko,
Matope na nawe yamesomba miteremko,
Geuza hali hii kuwa ile ya kutembea juu ya maji katika Bahari ya Galilaya
Yesu Una nguvu Hadi ulaya
Wewe ni Yesu wa miujiza
Wewe ni suluhisho kwa matatizo yote duniani,
Na neno lako asilani
Linaweza kugeuza hali Fulani
Kutoka kuwa mbaya Hadi ya furaha
Wakati nimekumbwa na hofu,
Siwezi hata kumudu karo ya shule wala kupata minofu,
Hela hakuna hata ya kunulia watoto vibofu,
Geuza hali hii kuwa ile ya kutuliza dhoruba,
Kemea upepo wa hofu.
Itulize roho jinsi wafuasi wako walivyotulia
Wewe ni Yesu wa miujiza.
Wewe ni suluhisho kwa matatizo yote duniani,
Na neno lako pekee
Linaweza kugeuza hali
Kutoka mbaya na kuifanya ya furaha
Ugonjwa unaponishusha hadhi chini,
Nazungushwa hospitalini Hadi hospitalini,
Nazungushwa hospitali Zote nchini,
Ninageuka mwenye hela Hadi maskini,
Geuza hali hii kuwa kama ile ya kumponya yule aliyepooza,
Hata nikija kupitia juu ya paa!
Wewe ni Yesu wa miujiza.
Wewe ni suluhisho kwa matatizo yote duniani,
Na neno lako asilani
Linaweza kugeuza hali fulani
Kutoka mbaya na kuifanya ya furaha.
Macho yangu yanaponishinda kabisa,
Kutoa machozi Hadi siwezi soma kurasa,
Yesu njoo unipige msasa wa kisasa.
Niwe nami naweza kusoma Kwa darasa,
Geuza hali hii kuwa kama ile ya Bartimayo.
Aliyerejeshewa uwezo wake wa kuona.
Wewe ni Yesu wa miujiza.
Wewe ni suluhisho kwa matatizo yote duniani,
Na neno lako asilani
Linaweza kugeuza hali Fulani,
Kutoka mbaya na kuifanya ya furaha.
Yesu ni nguzo
Yesu ni suluhisho la matatizo,
Yesu ni chetezo,
Yesu ana uwezo.