A song made by Owiti Arwa Chitu
A song made by Owiti Arwa Chitu
Chituz,
Na Afrobits
MZEE KONYEZO
Katika kijiji kilichojulikana kama Koroboi,
Paliishi Mzee aliyependa Sana kuvaa kikoi,
Mzee mwenye roho chafu,
Roho iliyojaa kutu,
Roho ya kufikiria maovu,
Wivu mwingi ya kiuchawi uchawi!
Jina lake alijulikana kama Mzee KONYEZO!
Mzee KONYEZO akikonyeza Tu!
Baya Lazima litampata MTU,
Awe mama,Baba,mtoto au ajuza,
Wote Mzee kikomo nyota zao alikatiza.
NI Mzee mjuaji,kimbelembele,
Mashamba ya watu alinyakua si nyuma wala mbele,
Ukimpinga utapata mwili wako umevamiwa na vipele,
Kumbe Mzee KONYEZO ashakurushia mchele,
Maovu Yake yalikuwa teletele!
Jina lake alijulikana kama Mzee KONYEZO.
Mzee KONYEZO akikonyeza Tu!
Baya Lazima litampata MTU,
Awe mama,Baba,mtoto au ajuza,
Wote Mzee kikomo nyota zao alikatiza.
Kulikuwa na mtoto aliyekuwa msomi,
Alidibua vitabu vya kila ndimi,
Sifa zake zilienea si kijijini Hadi mjini,
Kumbe Mzee KONYEZO kampangia wale waovu majini,
Siku ya mtihani kufika,
Mtoto mtahiniwa hakuweza kusoma matini!
Jina lake alijulikana kama Mzee KONYEZO.
Mzee KONYEZO akikonyeza Tu!
Baya Lazima litampata MTU,
Awe mama,Baba,mtoto au ajuza,
Wote Mzee KONYEZO nyota zao alikatiza.
Kuna Baba aliyepandishwa cheo,
Watu walifurahia kwake kufika upeo,
Kijiji kikapanga kupiga bonge la sherehe,
Mzee KONYEZO alipopata habari,
Akahapa kuwa hawataona fahari,
Siku ya sherehe jamaa aligeuka chizi,
Alipatikana chini ya Mgomba WA ndizi!
Jina lake alijulikana kama Mzee Konyezo
Mzee KONYEZO akikonyeza Tu!
Baya Lazima litampata MTU,
Awe mama,Baba,mtoto au ajuza,
Wote Mzee KONYEZO nyota zao alikatiza.
Uwe mama aliye Kwa njia ya uzazi,
Mzee KONYEZO atakutafutia vazi,
Liwe rinda, sharti au jezi,
Mzee KONYEZO atakuwekea kiunzi!!
Ukivaa Tu! Umeavya!
Jina lake alijulikana kama Mzee KONYEZO.
Mzee KONYEZO akikonyeza Tu!
Baya Lazima litampata MTU,
Awe mama,Baba,mtoto au ajuza,
Wote Mzee KONYEZO nyota zao alikatiza.
Kwakuwa siku za mwizi NI arubainne,
Mzee KONYEZO alirusha ndhumba Kali,
Kwa mtoto mahafali, aliyekuwa WA mjane mwombaji na aliyependa kufunga na kuomba,
Ndhumba Zote zilimrudia KONYEZO!
Yale yote ambayo asharusha yakamrudia,akiwa Kwa shamba,
Alijipata NI kipofu,kiziwi,Kiwete,bubu na pia mwenye akili tahira!
Na wote aliowaroga wakapata nafuu!
Mungu kweli si Athumani!
Jina lake alijulikana kama Mzee KONYEZO.
Mzee KONYEZO akikonyeza Tu!
Baya Lazima litampata MTU,
Awe mama,Baba,mtoto au ajuza,
Wote Mzee KONYEZO nyota zao alikatiza.
Tuwacheni ukonyezo
Tuwacheni ukonyezo
Tuwacheni ukonyezo
Tuwacheni ukonyezo