A song made by Sir Nixy
A song made by Sir Nixy
intro
Sir Nixy
"Yeah...
Kila nikijaribu kusimama,naangushwa chini..
Nilibadili majina,nikadhani nitabadili na maumivu...
Kumbe ni walewale..."
"Ooooh...mmmh...
Valentine alinifanya nilie...
Mariam akaniacha gizani...
Hata Blessings...ukataka kutoa roho yangu?
Hehe..
Dah...mapenzi basi..."
Verse 1
Nilitia nia nikafungua na mlango
Kila nikipenda,mwisho wake ni masikitiko
Moyo umeshachoka kuwa uwanja wa mapambano
Kila mwanamke kwangu amekuwa shindano
Wamekua kama ndege tunduni,nawafananisha
Kila nikijaribu kushika,wanaruka na kunitupa
Nikawa mtumwa wa machozi,nalia kila kukicha
Huu mchezo wa kupenda,unaumiza sana.
Verse 2
Alianza Valentine,jina lake likanidanganya
Nikadhani atakua wangu wa daima,moyoni nikamfunga
Haikupita hata miezi,akili akageuza
Alisomba kila kitu ndani,nyumba akaiacha tupu,akatokomea.
Nikasema isiwe tabu,majeraha nikayafuta
Nikamfuata Mariam,nikajua hapa sasa nimefika
Kama mamake Yesu,ufalme wa amani nimeukuta
Kumbe umbwa mwitu,usiku wa giza akanitoroka
Bila hata mbalamwezi,amani yangu akaivuruga.
Chorus
Kama mapenzi ni kitu kizuri,mbona yanifanye nilie ?
Kama mapenzi ni kitu tamu,mbona yatese mimi pekee?
Mimi mapenzi basi! Sililii tena mapenzi!
Sitaki kupenda,na sitaki kupendwa!
Nimebaki na kovu la mapenzi...rohoni mwangu.
Nimebaki na kovu la mapenzi...sitaki tena.
Verse 3
Moyo ukaona upweke,nikadhani nitapata bahati
Nikampata Blessings,akaja na maneno ya ushawishi
Akasema yeye ni baraka,tofauti na wale wa mwanzo
Akaniahidi paradiso,kumbe ananivuta motoni
Huyu sasa nusra aitoe kabisa roho yangu
Niliamkia hospitali,baada ya siku tatu za giza tupu
Daktari akaniambia,nilipewa sumu kali mwilini mwangu
Mpenzi niliyemwamini,alitaka kunizika nikiwa hai..
Chorus
Kama mapenzi ni kitu kizuri,mbona yanifanye nilie ?
Kama mapenzi ni kitu tamu,mbona yatese mimi pekee?
Mimi mapenzi basi! Sililii tena mapenzi!
Sitaki kupenda,na sitaki kupendwa!
Nimebaki na kovu la mapenzi...rohoni mwangu.
Nimebaki na kovu la mapenzi...sitaki tena.
Bridge
Nilitoa upendo wa dhati,nikalipwa kwa usaliti
Nilitafuta faraja,nikavuna mauti
Moyo wangu sasa nijiwe,hauhisi tena mapenzi
Fungeni milango,nishafunga na duka la hisia...
Outro
Basi nenda...valentine nenda...
Mariam nenda... Blessings nenda kabisa...
Mimi na mapenzi hatuendani,kovu lishakuwa kubwa.
Sitaki kupenda...sitaki kupendwa
Mmmmh..
Sir Nixy.