[male vocals] WCB!
Twende!
Siku
hizo
Hezekia
aliugua,
akawa
katika
hatari
ya
kufa;
na
Isaya
nabii,
mwana
wa
Amozi,
akaenda
kwa
mfalme,
akamwambia,
Bwana
asema
hivi,
Tengeneza
mambo
ya
nyumba
yako;
maana
utakufa,
wala
hutapona.
Basi
Hezekia
akajigeuza,
akaelekeza
uso
wake
ukutani,
akamwomba
Bwana,
akasema,
Ee
Bwana,
kumbuka
haya,
nakusihi,
kwamba
nimekwenda
mbele
zako
katika
kweli
na
kwa
moyo
mkamilifu,
na
kutenda
yaliyo
mema
machoni
pako.
Hezekia
akalia
sana
sana.
Ikawa,
neno
la
Bwana
likamjia
Isaya,
kusema,
Enenda
ukamwambie
Hezekia,
Bwana,
Mungu
wa
Daudi,
baba
yako,
asema
hivi,
Mimi
nimeyasikia
maombi
yako,
nimeyaona
machozi
yako;
tazama,
nitaziongeza
siku
zako,
kiasi
cha
miaka
kumi
na
mitano.
Nami
nitakuokoa
wewe,
na
mji
huu,
na
mkono
wa
mfalme
wa
Ashuru,
nami
nitaulinda
mji
huu.
Jambo
hili
liwe
ishara
kwako,
itokayo
kwa
Bwana,
ya
kuwa
Bwana
atalitimiza
jambo
hili
alilolisema;
Tazama,
nitakirudisha
nyuma
kivuli
madaraja
kumi,
ambayo
kilishuka
juu
ya
duara
ya
Ahazi
kwa
sababu
ya
jua.
Basi
jua
likarudi
madaraja
kumi
katika
hiyo
duara,
ambayo
limekwisha
kushuka.
Haya
ndiyo
maandiko
ya
Hezekia,
mfalme
wa
Yuda,
alipokuwa
hawezi,
naye
akapona
ugonjwa
wake.
Nalisema,
Katika
usitawi
wa
siku
zangu
nitakwenda
kuingia
malango
ya
kuzimu;
Nimenyimwa
mabaki
ya
miaka
yangu.
Nalisema,
Sitamwona
Bwana,
yeye
Bwana,
katika
nchi
ya
walio
hai;
Sitamwona
mwanadamu
tena
pamoja
na
hao
wakaao
duniani.
Kao
langu
limeondolewa
kabisa,
limechukuliwa
kama
hema
ya
mchungaji;
Nimekunja
maisha
yangu
kama
mfumaji;
atanikatilia
mbali
na
kitanda
cha
mfumi;
Tangu
mchana
hata
usiku
wanimaliza.
Nalijituliza
hata
asubuhi;
kama
simba,
aivunja
mifupa
yangu
yote;
Tangu
mchana
hata
usiku
wanimaliza.
Kama
mbayuwayu
au
korongo
ndivyo
nilivyolia;
Naliomboleza
kama
hua;
macho
yangu
yamedhoofu
kwa
kutazama
juu;
Ee
Bwana,
nimeonewa,
na
uwe
mdhamini
wangu.
Niseme
nini?
Yeye
amenena
nami,
na
yeye
mwenyewe
ametenda
hayo;
Nitakwenda
polepole
miaka
yangu
yote,
kwa
sababu
ya
uchungu
wa
nafsi
yangu.
Ee
Bwana,
kwa
mambo
hayo
watu
huishi;
Na
uhai
wa
roho
yangu
u
katika
hayo
yote;
Kwa
hiyo
uniponye
na
kunihuisha.
Tazama;
nalikuwa
na
uchungu
mwingi
kwa
ajili
ya
amani
yangu;
Lakini
kwa
kunipenda
umeniokoa
na
shimo
la
uharibifu;
Kwa
maana
umezitupa
dhambi
zangu
zote
nyuma
yako.
Kwa
kuwa
kuzimu
hakuwezi
kukusifu;
mauti
haiwezi
kukuadhimisha;
Wale
washukao
shimoni
hawawezi
kuitarajia
kweli
yako.
Aliye
hai,
naam,
aliye
hai,
ndiye
atakayekusifu,
kama
mimi
leo;
Baba
atawajulisha
watoto
kweli
yako.
Bwana
yu
tayari
kunipa
wokovu.
Basi,
kwa
vinubi
tutaziimba
nyimbo
zangu,
Siku
zote
za
maisha
yetu
nyumbani
mwa
Bwana.
Maana
Isaya
amesema,
Na
watwae
mkate
wa
tini,
wakauweke
juu
ya
jipu,
naye
atapona.
Tena
Hezekia
alikuwa
amesema,
Iko
ishara
gani
ya
kunionyesha
ya
kuwa
nitapanda
niingie
nyumbani
mwa
Bwana?