A song made by Owiti Arwa Chitu
A song made by Owiti Arwa Chitu
MATATU HAZINA MATATA
Utunzi WA Owiti Arwa Chitu
Matatu hazina MATATA
Ila utata unaletwa na waabiri na wasioabiri matatu.
Sisi wanamatatu KAZI yetu twaienzi,
Japo hatusubiri Hadi mwisho WA mwezi,
NI vyema kujua Sisi si Wezi wala majambazi,
Bali Sisi NI wazazi wanaopenda
Yao KAZI
Kwa hakika Matatu hazina MATATA
KAZI yetu riziki twapata
Na wasafiri haki wanapata,
Hii NI KAZI si kubeti kama vile karata.
Jasho letu hapa twalitoa,
Nauli lipa hii si KAZI ya Shokoa,
Ukikwama njiani NI Sisi twakuokoa
Viti tumeunda ukikaa wasikia Tu poa,
Si kupenda kwetu sambaza kutoa,
Kwa hakika Matatu hazina MATATA
KAZI yetu riziki twapata
Na wasafiri haki wanapata,
Hii NI KAZI si kubeti ama karata.
Gange hii familia yasubiria
Tafadhali ndugu yangu abiria
Jinsi unavyoenda kazini jua nasi pia,
Hapa ndio kuna mlo
Hapa ndio kuna Karo
Hapa ndio malazi ya watoto kudoro,
Hapa ndio mavazi yanatoka usiwe na tofauti michoro,
Kwa hakika Matatu hazina MATATA
KAZI yetu riziki twapata
Na wasafiri haki wanapata,
Hii NI KAZI si kubeti ama karata.
Hali ya maisha imepanda,
Uwe Mwalimu, rubani au mpiga Randa,
Basi Kwa nini Mimi hutaki kunifungia mkanda,
Ilhali nateremka nawe milima na pia ukipanda,
Nifae ili Mimi presha isijeikapanda,
Ifikapo TAREHE kumi na NNE kila mwezi......mishipa ya damu yanadinda,
Kwa hakika Matatu hazina MATATA
KAZI yetu riziki twapata
Na wasafiri haki wanapata,
Hii NI KAZI si kubeti ama karata.
Hapa tuko watatu,
Kuna Mimi dereva WA Matatu,
Kuna kondakta tunayesafiri naye
Kisha kuna anayebaki,aendi yeye
Al maarufu-Manamba,
Hata kama Hana namba,
Chunga Sana asijeakakuramba,
KAZI Yake NI muhimu Kwa hili shamba.
Kwa hakika Matatu hazina MATATA
KAZI yetu riziki twapata
Na wasafiri haki wanapata,
Hii NI KAZI si kubeti ama karata.

Pick one photo or multiple for a slideshow (up to 10) — we'll create a video with your track, ready for TikTok, Reels & Stories
Opening gallery…
Select your photo
Cooking your video...
We'll send it straight to you when it's hot 🔥
You can close this page — we'll deliver it directly to you.
Your video is ready!
It's been sent to your WhatsApp. Save it, then post it to your socials below.
Tag @afrobits.ai when you post
Get your own artist profile on Spotify, Apple Music & 150+ platforms. First song included — add more for just each.
Millions of listeners are waiting to hear your sound
Annual subscription · First song included · Add more songs for just each · Cancel anytime
Annual subscription. Auto-renews yearly. Cancel anytime — your song stays live until the paid period ends.