A song made by Mwana Emanuel
A song made by Mwana Emanuel
WIMBO WA GRADUATION – CALVARY SCHOOL OF MINISTRY
Tuko mbele zako, ee Mungu Baba yetu,
Tunainua sifa, tunakupa utukufu.
Leo twasimama kwa neema yako,
"Mimi hapa Bwana, nitume mimi!"
Roho Mtakatifu, tuongoze daima.
Tuko mbele zako, ee Mungu Baba yetu,
Mbele ya mchungaji wetu kiongozi, Philip David.
Tumezungukwa na mashahidi wengi wa imani,
Tukiitika wito wa kutumwa,
Kuwa walimu wa Neno lako la uzima.
Haya ndiyo malimbuko ya maono ya
Calvary School of Ministry.
Kwa uongozi wa mtumishi wako,
Mchungaji Philip David,
Tumesimama tayari kusema:
"Mimi hapa Bwana, nitume mimi!"
Kwa msaada wa Roho Mtakatifu.
Agnes Thomas Tarimo,
Allan Eniyoye Mhiro,
Anjela Petro Karoli,
Emmanuel Gervas Tarimo,
Emanuel Edward Mwanakadudu.
Faith Elingaya Munissi,
Frajeth Focus Felesian,
George Ambaeli Kimaro,
Glory S. Martin,
Godbless Tito Nkya.
Hekima Abel Munguwamajeshi,
Linus E. Mallya,
Maria Daniel Swai,
Mathew Joseph Lyatuu,
Miriam Joseph Sokko.
Samwel Micah Gunda,
Simon Baha Panga,
Solomon Temanyika Kiondo,
Terry Wilson Kimaro,
Witness Samson Munisi.
Sote kwa sauti moja twasema:
"Mimi hapa Bwana, nitume mimi!"
Tumefundishwa Neno la kweli,
Tumekuzwa katika hekima na maarifa.
Kutunga na kuhubiri hotuba,
Kutafsiri Maandiko Matakatifu,
Kutambua na kupinga mafundisho potofu.
Tumejifunza Misheni ya Mungu,
Na mengi yenye kulijenga Kanisa lake.
Sasa tuko tayari kutumwa duniani.
Asante Baba yetu, Mchungaji Philip David,
Asante Mama yetu, Mchungaji Pamela.
Kwa upendo, maombi na uongozi wenu,
Mungu awalipe kwa wema wake.
Asante wakufunzi wetu waaminifu:
Mchungaji Charles Kimaro,
Mchungaji Jane Kombe,
Dkt. Masanja,
Dkt. Adela Materu.
Bwana awabariki sana!
Twende kwa nguvu za Roho,
Twende kuhubiri Injili ya Kristo.
Kanisa lijengwe, mataifa yaokolewe,
Jina la Yesu litukuzwe milele.
Tuko mbele zako, ee Mungu Baba yetu,
Tunainua sifa, tunakupa utukufu.
Leo twasimama kwa neema yako,
"Mimi hapa Bwana, nitume mimi!"
Amina! Amina! Haleluya!