A song made by Sir Nixy
A song made by Sir Nixy
Sir Nixy
Yeah...Uhm
Barua ya majonzi ya mzee Tingatinga kwa mke wake na wanawe akiwa Hospitalini!..
Daktari anasikika akimwambia Nesi!
"Ongeza hewa ya oksijeni haraka,presha yake ipo juu sana na sukari imeshuka kabisa! Mpigie simu mke wake au watoto wake waje haraka,huyu mzee anapoteza fahamu..."
Nesi akajibu akisema,"Daktari, nimepiga simu zote...mke wake na watoto wamekataa,wanasema hawamjui huyu mzee na tusiwasumbue..."
Mzee Tingatinga anakohoa
(Kuh! Kuh!)
Nakusema!...
Nalia mimi,.hi!..hi!..hi!.."Hata nyinyi wanangu?...Sawa...Ooh mungu wangu..."
Nilitembea peku,miguu imejaa makovu,
Nguo zimechanika,nikaitwa mchafu mchovu.
Kila senti niliyopata,nikaweka kwenye elimu yenu.
Mke wangu nikampandisha,nikachukua madeni ya benki,
Nikamfungulia biashara,leo hii hanitambui hata chembe.
Amewalisha sumu wanangu,mnaona mi sifai,
Mzee wenu nimebaki takataka,mnatamani hata nisivute hai.
Mwili wangu unawaka moto,sukari inaniramba mifupa!
Presha inapanda kwa uchungu,mzee wenu mumenitupa!
Mbona mwanilisha miiba,wakati niliwapa mkate?
Mbona mwaninyima hewa,mnataka mzee wenu nife kwa mate?
Machozi yangu ya damu,yanalia ardhini,
Mnafurahi mjini,mimi mumenizika nikiwa hai bandani!
Mimi ni kama Tingatinga(excavator)...ooh...
Nimesafisha pori,nikasawazisha milima na mawe,
Nikatengeneza barabara,ili nyinyi mpite kwa amani.
Leo barabara imekamilika,mnaendesha magari ya kifahari,
Lakini mimi mzee wenu,mnasema nitaleta uharibifu...siruhusiwi kupita!
Mumenitupa kando ya njia,mkanisahau kabisa,
Kwenye barabara ile ile,niliyoteseka kujenga.
Sasa hivi nime-retire,Nguvu zote zimeisha,
Sukari na presha mwilini,ndio vitu vinavyonisaidisha.
Miguu imevimba,mishipa inanichoma kama moto,
Sina hata mia ya vidonge,huku nikitetemeka kwa baridi ya usiku kucha.
Lile banda la mbuzi mlilonitupa kijijini,
Nzi na wadudu ndio marafiki zangu gizani.
Mke wangu uliuza zile nyumba za kupanga,
Ukaenda town kula raha na wanangu,mzee wenu mkaniacha ninafanya tangatanga.
Mwili wangu unawaka moto,Sukari inaniramba mifupa!
Presha inapanda kwa uchungu,mzee wenu mumenitupa!
Mbona mwanilisha miiba,wakati niliwapa mkate?
Mbona mwaninyima hewa,mnataka mzee wenu nife kwa mate?
Machozi yangu ya damu,yanalia ardhini,
Mnafurahi mjini,mimi mumenizika nikiwa hai bandani!
Mwili unatetemeka(kwa baridi)...
Dawa sina...Chakula sina...
Mke niliyekupa heshima,leo unanicheka nikiwa hai?
Mungu wangu nionee huruma,pumzi inakata...
Tingatinga lenu limechoka...
Barabara mnafurahia...lakini muumbaji anaona.
Mungu awasamehe...wanangu...mke wangu...