A song made by Owiti Arwa Chitu
A song made by Owiti Arwa Chitu
Chituz
WALIKUTANA MTANDAONI
Amina wa mitandaoni.......
Kwa mtandao Sura yake ilikuwa vutifu,
Kwa vitengo vya mitandao usingejua sura NI chafu,
Alifuatwa, liked,hadi na machifu,
Ungeona Sura Kwa mtandao Sawa na ya malaika mtakatifu,
Likes zake kila mahali hazikuwa hafifu,
Kwakuwa kila zuri lavutia,
Alimpata Tajiri Fuadi, fulusi,pesa Kwa wingi akamvutia,
Walikutana Mitandaoni.
Kitengo cha WhatsApp -Amina alikuwepo.
Ukienda Kwa Facebook -Amina yupo yupo.
Kitengo cha Istagramu-Amina Yuko topu.
Walikutana mitandaoni
Amina alipendezwa na pesa na mwonekano wa Tajiri Fuadi,
Fuadi alimtunuku Amina Ile ghali Kadi,
Kadi ya hela nyingi akaanza miradi,
Miradi ikanawiri akawahusisha kina Amadi,
Kisha zikaanza zile mbaya itikadi.
Walikutana Mitandaoni.
Kitengo cha WhatsApp -Amina alikuwepo.
Ukienda Kwa Facebook -Amina yupo yupo.
Kitengo cha Istagramu-Amina Yuko topu.
Walikutana Mitandaoni.
Sura Yake Amina ya Mitandaoni,
Ilikuwa tofauti Sana na Ile ya 'ground' yaani uwanjani,
Fuadi alijua fika kuwa huu ni mchezo na utani,
Lakini alielewa vizuri na akapanga mpango Fulani,
Alikuwa na biashara yake ya figo,moyo na maini,
Walikutana mitandaoni
Kitengo cha WhatsApp -Amina alikuwepo.
Ukienda Kwa Facebook -Amina yupo yupo.
Kitengo cha Istagramu-Amina Yuko topu.
Walikutana Mitandaoni
Kundi la Amina likazidi kuongezeka,
Amina alipumbaza wengi na sura ya mtandao na kuwashika,
Aliingia Kwa vikasha yaani inbox bila kubabaika,
Hela alizopewa wengi walienda kuburudika,
Kumbe hawakujua kile ambacho kitawafika,
Walikutana mitandaoni
Pole pole na taratibu wanachama wakaanza kupotea,
Malipo ya Kula vya bure sasa wakaanza kupokea,
Mmoja alikunywa Sana akaanguka,
Wezi walimpata njiani wakamsaka,
Maini,figo na moyo walizitwika,
Mmoja baada ya mwengine kifo kiliwafika.
Walikutana Mitandaoni.
Kitengo cha WhatsApp -Amina alikuwepo.
Ukienda Kwa Facebook -Amina yupo yupo.
Kitengo cha Istagramu-Amina yuko topu.
Walikutana Mitandaoni
Mwisho wa mitandaoni mrembo,
Pia naye akajipiga nyingi tembo,
Baadaye alipatwa katika chumba fulani,
Mrembo katobolewa kila sehemu mwilini,
Bila hata sehemu za ndani kama maini,
Walikutana Mitandaoni
Kitengo cha WhatsApp -Amina alikuwepo.
Ukienda Kwa Facebook -Amina yupo yupo.
Kitengo cha Istagramu-Amina yuko topu.
Walikutana Mitandaoni.
Mwisho wa siku Amina mrembo aliiaga dunia,
Urembo wake wote wa mitandaoni aliitwa Kwa gunia,
Mivutio ya Mitandaoni ina mipaka,
Wengi ni watakurusha Kwa takataka.
Mwili wako wakuache wameukatakata!!
Walikutana Mitandaoni
Kitengo cha WhatsApp -Amina alikuwepo.
Ukienda Kwa Facebook -Amina yupo yupo.
Kitengo cha Istagramu-Amina yuko topu.
Chunga Sana
Unapouza sura Mitandaoni,
Kuna kina Fuadi,
Wanataka nyingi fuadi!
Maini,figo na damu!
Amina mrembo WA mitandaoni.