A song made by Man Of God's Chris Msaki🙏
A song made by Man Of God's Chris Msaki🙏
Chriss Msaki naomba Leo Bwana pokea Sifa Zako wewe ni Mungu wa kweli na unatenda Mema katika Maisha yetu.
Chouras
Usifiwe Mungu wa Isaka baba
Usifiwe Mungu wa Yaboko baba
Usifiwe Mungu wa Isaka baba x 4
Verse
Nalisifu jina lako masiya yawe (Yawe)
Nalisifu jina lako masiya Yawe (yawe)
Wewe ni baba Yawe
Wewe ni Mungu Yawe
Chris Msaki nasimulia kwa mataifa yote jinsi wewe ulivyo mkuu na matendo yako makuu haulinganishwi na chochote kile pokea Sifa Baba 1Msifuni Mwenyezi-Mungu!
Msifuni Mungu katika patakatifu pake;
msifuni katika mbingu zake kuu.
2Msifuni kwa sababu ya matendo yake makuu;
msifuni kwa ajili ya utukufu wake mkuu.
3Msifuni kwa mlio wa tarumbeta;
msifuni kwa zeze na kinubi!
4Msifuni kwa ngoma na kucheza;
msifuni kwa filimbi na banjo!
5Msifuni kwa kupiga matoazi.
Msifuni kwa matoazi ya sauti kubwa.
6Kila kiumbe hai kimsifu Mwenyezi-Mungu!
Msifuni Mwenyezi-Mungu! Chris Msaki nalisifu jina Lako Bwana hallelujah
Nitamhimidi Bwana kila wakati, Sifa zake zi kinywani mwangu daima.
Atoaye dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza. Naye autengenezaye mwenendo wake, Nitamwonyesha wokovu wa Mungu. - Zaburi 50:23
Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake. Msifuni kwa matendo yake makuu; Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake. Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi; Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi; Msifuni kwa matoazi yaliayo; Msifuni kwa matoazi yavumayo sana. Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana. Haleluya.
Heri watu wale waijuao sauti ya shangwe, Ee Bwana, huenenda katika nuru ya uso wako.
Mfanyieni Bwana shangwe, dunia yote; Mtumikieni Bwana kwa furaha; Njoni mbele zake kwa kuimba;
Ni neno jema kumshukuru Bwana, Na kuliimbia jina lako, Ee Uliye juu.
Rehema na hukumu nitaziimba, Ee Bwana, nitakuimbia zaburi.
Bwana ametamalaki, nchi na ishangilie, Visiwa vingi na vifurahi.
Enyi wenye haki, mmfurahieni Bwana, Na kulishukuru jina lake takatifu. - Zaburi 97:12
Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Naam, vyote vilivyo ndani yangu Vilihimidi jina lake takatifu. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, Wala usizisahau fadhili zake zote.
Na walisifu jina lake kwa kucheza, Kwa matari na kinubi wamwimbie. Kwa kuwa Bwana awaridhia watu wake, Huwapamba wenye upole kwa wokovu. Watauwa na waushangilie utukufu, Waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao.
Atoaye dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza. Naye autengenezaye mwenendo wake, Nitamwonyesha wokovu wa Mungu.
Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza.
Naye alipokwisha kufanya shauri na watu, akawaweka wale watakaomwimbia Bwana, na kumsifu katika uzuri wa utakatifu, wakitoka mbele ya jeshi, na kusema, Mshukuruni Bwana; kwa maana fadhili zake ni za milele. Nao walipoanza kuimba na kusifu, Bwana akaweka waviziao juu ya wana wa Amoni, na Moabu, na wa mlima Seiri, waliokuja juu ya Yuda; nao wakapigwa.
shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.
Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamayo jina lake.
Kinywa changu kitajazwa sifa zako, Na heshima yako mchana kutwa.
Nami nitatumaini daima, Nitazidi kuongeza sifa zake zote.
Toka maawio ya jua hata machweo yake Jina la Bwana husifiwa.
mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo; -
Sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumwa wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo kwa wakuu. -