A song made by Sir Nixy
A song made by Sir Nixy
Yeah...mmh..
Sir Nixy ..
Salma malkia wangu,mbona unanitesa akili?
Upendo gani huu unaoniumiza mwili?
Nataka uende...lakini nataka ubaki.
Dah! Moyo unafanya mapinduzi, ooh Salma...
Urembo wako tishio,Sura kama malaika
Ukitembea barabarani,macho yote yanakufuata
Lakini uzuri wako Salma,kwangu umekua donda
Ukitoka tu kidogo,roho inaanza kudunda
Umechelewa sokoni,masaa yanavyosogea
Wazimu unanipanda,picha mbaya nazionea
Naona kama uko kwa mume mwingine unacheka
Kitandani nakosa amani,jasho linanitiririka.
Ofisini kwenu ndo kabisa,sielewi Salma
Ukicheka na machali wa kazi,nakua mlevi
Juzi boss wako amekushusha na lile gari
Pressure ilipanda,nikahisi hatari
Hata Baba Joan jirani,alipokuambia "Happy Mothers Day"
Nilihisi usaliti,nikasema leo "No way Salma"
Moyo unasema uende,nishachoka na stress
Kila saa naona naibiwa,niko radhi nibaki peke yangu
Lakini nikikumbuka yale mapenzi matamu ya Salma
Narudisha chini roho,nanywa sumu ya Kalamu
Nimesema uishie...ila nikiiona hiyo figure
Upendo unanirudia,natamani ubaki kigori
Aah,nenda Salma ! Hapana... baki!
Huu wivu utanitoa roho.
Niliamua leo hii ndoa yetu ifike kikomo
Ufunge virago vyako,utoke kwenye langu lango
Uende mbali kabisa Salma,usionekane na macho yangu
Ila picha yako akilini,bado ni msumari kwangu
Jana nimekuona mjini,mwanaume amekushika mkono
Wivu ulinijaa kifuani,nilitamani kuanzisha mzozo
Nilitaka kuwavamia,niwapige niwaondoe
Lakini nikakumbuka sura ya Salma,nikajikuta nanyamaza tu nichezee.
Ooh Salma...urembo wako ni mtego
Unanichanganya akili,unavunja zangu ngano
Nataka utokomee,lakini siwezi pumzi kuvuta
Bila wewe mpenzi,maisha yangu yanafilisika.
Hivi ni mapenzi gani haya yanayouma hivi?
Natamani kukuacha Salma,lakini siwezi hata sekunde
Uzuri wako ni jela yangu,na mimi ndio mfungwa
Kila nikisema "Basi!" umbo lako linanitunza
Nateseka...naumia...
Nataka uende Salma,lakini usiondoke!
Moyo unasema uende,nishachoka na stress
Kila saa naona naibiwa,niko radhi nibaki peke yangu
Lakini nikikumbuka yale mapenzi matamu ya Salma
Narudisha chini roho,nanywa sumu ya kalamu
Nimesema uishie...ila nikiiona hiyo figure
Upendo unanirudia,natamani ubaki kigori!
Aah,Nenda Salma! Hapana...baki!
Huu wivu utanitoa roho.
Uende...au ubaki Salma?
Malkia wangu wa nguvu...
Huu wivu ni ugonjwa,na dawa ni wewe tu.
Baki basi mrembo wangu...lakini usichelewe sokoni tena.
Yeah...Oh Salma...
Sir Nixy...