A song made by Mwl. Imani Nyingi
A song made by Mwl. Imani Nyingi
YESU NI MLANGO WA KUINGIA MBINGUNI
Yesu ndiye Mfalme, ndiye njia kweli na uzima.
Yesu ni Mlango
Mlango wa kuingia Mbinguni
Onjeni muone
Ya kwamba yeye ni mwema
Na fadhili zake ni za milele haleluya haleluya haleluya
Mungu, njia yake ni kamilifu,
Ahadi ya BWANA imehakikishwa,
Yeye ndiye ngao yao.
Wote wanaomkimbilia.
Maana ni nani aliye Mungu ila BWANA?
Ni nani aliye mwamba ila Mungu wetu?
Mungu ndiye anifungaye mshipi wa nguvu,
Naye anaifanya kamilifu njia yangu.
Miguu yangu anaifanya kuwa ya kulungu,
Na kunisimamisha mahali pangu pa juu.
Ananifundisha mikono yangu vita,
Mikono yangu ikaupinda upinde wa shaba
Nawe umenipa ngao ya wokovu wako,
Mkono wako wa kuume umenitegemeza,
Na unyenyekevu wako umenikuza.
Umezifanyizia nafasi hatua zangu,
Na miguu yangu haikuteleza.
Yesu ndiye Mfalme, ndiye njia kweli na uzima.
Yesu ni Mlango
Mlango wa kuingia Mbinguni
Onjeni muone
Ya kwamba yeye ni mwema
Na fadhili zake ni za milele haleluya haleluya haleluya
Nasi tulikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zetu;
Ambazo tuliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu,
na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa
katika wana wa kuasi;
ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao,
katika tamaa za miili yetu,
tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine.
Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda;
hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani,
Tumeokolewa kwa neema.
Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho,
katika Kristo Yesu;
ili katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu.
Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo
haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;
wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.
.
Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.
Sote tutende haki yake
Yeye anasema
"Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.
Yesu ndiye Mfalme, ndiye njia kweli na uzima.
Yesu ni Mlango
Mlango wa kuingia Mbinguni
Onjeni muone
Ya kwamba yeye ni mwema
Na fadhili zake ni za milele haleluya haleluya haleluya